MANISPAA ya Kinondoni inatarajia kufanya operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara waliopo katika eneo la Kituo cha Daladala cha Mwenge na Tegeta wakati wowote kuanzia leo, ikiwa ni muendelezo wa operesheni yake kwa wafanyabiashara waliopo katika hifadhi za Barabara.
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka kwa mmoja wa maofisa wa manispaa hiyo ambaye hata hivyo hakupenda kutaja jina lake, ilisema kwa sasa uongozi wa manispaa hiyo upo kwenye vikao vya majadiliano juu ya operesheni hiyo, kabla ya kuanza rasmi kwa utekelezaji wake.
Gazeti hili lilipomtafuta Ofisa Habari wa Manispaa hiyo, Sebastian Mhowela, alikiri juu ya uwepo wa maandalizi ya operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara hao huku akiwataka wahusika wa biashara hizo kuondoka mapema ili kuepuka usumbufu wanaoweza kupata wakati wa operesheni hiyo.
“Kwa sasa ni kweli kuwa tupo katika kikao cha kuzungumzia operesheni hiyo hivyo siku yoyote itafanyika, lengo ni kuona kuwa maeneo yote ya wazi yanaachwa kama yalivyokuwa kabla ya kutokea kwa uvamizi huo,” alisema Mhowela.
Katika kipindi cha siku za hivi karibuni, manispaa hiyo kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, aliwataka wafanyabiashara walioko katika maeneo ya barabara kuondoka wenyewe, wakiwemo wa eneo la Ubungo ambao tayari wameshaondolewa
CHANZO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni