.........BLOG HII BADO IPO KWENYE MATENGENEZO......

Jumatano, 18 Aprili 2012

Mwakyembe, Makinda watema cheche bungeni

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe aliwataka wabunge kuwa makini na kusema heshima ya Tanzania ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kiasi imemomonyoka kwa kuwa baadhi ya wawakilishi wanakuwa chini ya viwango, wanakuwa mabubu kipindi chote cha uwakilishi wao.

Dk. Mwakyembe alisema alisema hayo baada ya baadhi ya wabunge kuonekana wakipinga uamuzi wa Spika wa kutaka wagombea wapewe dakika tano za kujieleza na kuulizwa maswali matatu.

Alisema taarifa za kuwepo rushwa kwenye mchakato ambazo zilitangazwa na vyombo vya habari, zinashusha heshima ya Bunge.

“Heshima yetu ndani ya jumuiya kwa kiasi imemomonyoka kutokana na baadhi ya wawakilishi kuwa chini ya viwango, wanakuwa mabubu kipindi chote cha uwakilishi wao. Watu wanajua kuomba kura na kupiga kura… Tuzingatie ushauri wa Spika,” alisema Mbunge huyo wa Kyela.

Akisisitiza kuwa maswali matatu yawe lazima, alisema na kama wabunge wengine watashindwa kuuliza waachiwe walimu (akiwemo) wawaulize wagombea.” Alikuwa miongoni mwa waliouliza maswali jana.

Spika Makinda alipigilia msumari kwamba wabunge waanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, akiwamo Dk. Mwakyembe walikuwa daraja la kwanza.

Aidha, Spika alisema japokuwa haki na utashi wa kura uko mikononi mwa Mbunge, aliwataka waweke kipaumbele kwenye maslahi ya taifa badala ya siasa.

“Hawa ni mabalozi wetu, maslahi ya taifa yasipozingatiwa, itakula kwetu,” alisema.

Zanzibar nao walilia kiti Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim Issa (CCM) alieleza kutofurahishwa na hatua ya Zanzibar kupewa nafasi mbili.

Alisema, “Napata mashaka yangu makubwa na historia niliyo nayo katika Bunge hili. Hatuna namna ya kuchanganyika baina ya Tanzania Bara tukawapigia kura kwa pamoja halafu Zanzibar ikaibuka ushindi. Inamaanisha kitendo kilichopita hapa ni kuwababaisha Wazanzibar.”

Wagombea na Kiingereza Wakati lugha ya kujieleza ilikuwa Kiingereza, mmoja wa wagombea, Rose Mwalusamba kutoka Chama cha Wananchi (CUF) alijitoa kwenye kinyang’anyiro baada ya kuwasili ukumbini na kutakiwa aanze kujieleza.

Baada ya kujieleza kwa Kiingereza kuwa taaluma yake ni uanasiasa, anaendesha kampuni inamwezesha kuwa na kipato, alitoa taarifa kwa Spika kwamba anataka kujiondoa.

(My profession is a politician…, I am coming from Mbeya CUF, I have a knowledge known as Political Science.., my daily bread….)

Mgombea Sophia Ali katika kujibu maswali, wakati mwingine Spika alilazimika kumfafanulia taratibu maswali kadhaa aliyoulizwa kabla ya kuondoka ukumbini akikimbia.

Awali, licha ya Spika Anne Makinda kuwakataza wabunge kushangilia, sharti hilo halikuzingatiwa baada ya baadhi ya wagombea kushangiliwa kutokana na ama majibu yao au namna walivyokuwa wakijieleza.
CHANZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni