.........BLOG HII BADO IPO KWENYE MATENGENEZO......

Jumanne, 24 Aprili 2012

Pinda aziba masikio mawaziri kujiuzulu



ALIPOULIZWA AKACHEKA, MKONO NAE AWEKA SAINI AONDOLEWE, UFISADI MALIASILI UNATISHA

WAKATI wabunge wakiendelea kusaini fomu ya majina ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni jana alikwepa kuzungumzia hatua za kinidhamu dhidi ya mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali.

Akiahirisha Mkutano wa Saba bungeni Dodoma, Pinda hakugusia suala la kujiuzulu kwa mawaziri wanane na badala yake alisema: “Siku zote Serikali imekuwa tayari kupokea ushauri wa Bunge baada ya kusikiliza mjadala na mapendekezo ya waheshimiwa wabunge.’’

Baada ya kuahirishwa kwa Bunge hadi Juni 12, mwaka huu. Pinda akiwa nje ya Bunge alikwepa kuzungumzia suala hilo licha ya kubanwa na waandishi wa habari na badala yake alicheka: "Haahaa," kisha akaingia kwenye gari na kuondoka.

Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema kitendo cha Pinda kushindwa kuzungumzia chochote kuhusu agizo la wabunge kutaka mawaziri wanane wawajibishwe, kimewaacha wananchi katika hofu.

Alisema Waziri Mkuu ametoa hotuba nyepesi kama vile taifa haliko katika giza kutokana na Bunge kutaka kuwajibishwa kwa mawaziri hao na kuapa kulifikisha suala hilo kwa wananchi.

“Aliahirisha shughuli za Bunge kama hakuna kitu kikubwa kilichohitaji majibu ya Serikali, wananchi walitaka kusikia mawaziri waliotajwa kwa tuhuma za ufisadi wakiwajibishwa lakini, hakuna chochote kilichofanyika. Sasa sisi tutakwenda kwa wananachi.

Jumamosi iliyopita, Pinda aliahidi kuwa jana Serikali ingeweka hadharani msimamo wake kuhusu suala baadhi ya mawaziri kutakiwa kujiuzulu lakini hakutekeleza ahadi yake.

Jana, Waziri Mkuu alisema Serikali itachukua hatua stahiki kuimarisha usimamizi na utendaji ndani ya wizara, Serikali za Mitaa na vyombo husika katika kuhakikisha watendaji wake wanafanya kazi kwa umakini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni