Leo ( Jana) ktk gazeti la Jambo Leo,ukurasa wa kwanza kuna kichwa cha habari kinachosema Chadema Inahusishwa na mashetani,na eti Dr.Slaa ana jini lake linalomsaidia mambo yake ya kisiasa,pia ktk dini hiyo kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Pope naye yumo.
Mwandishi amekwenda mbali zaidi kwa kumuhusisha Marehemu Kanumba na hiyo dini ya mashetani.Katika kujenga hoja amewaonyesha viongozi mbalimbali wa Dunia kuwa ni waumini wa dini hyo ya kishetani..Nimesikitishwa na umbumbumbu wa mwandishi,ujengaji wake wa hoja na zaidi kuwadhalilisha watu bila ushahidi wa kimantiki..msingi wa hoja yake kuwa Chadema na Dr.SLAA ni wafuasi wa shetani ni aina ya salamu ya vidole viwili inayotmiwa na Chadema,kuwa ni salamu ya kishetani na hivo Chadema ni ya mashetani na Dr.Slaa ana jini linalomlinda..
Kwa kweli huu ni upotoshaji mkubwa,haupaswi kuachwa,kulivamia pia kanisa kwa kumuhusisha kiongoz wao ni upotoshaji,ni kuuambia umma kuwa wote walio chini ya kiongozi huyo (Pope) nao ni waabudu sanamu!huu ni uzushi,uzandiki na ukomo wa uelewa wa mambo ya kidunia.
MY TAKE:...Alama ya "V" inayotumiwa na Chadema haina uhusiano na mashetani..miaka mingi iliyopita,Jemedari wa vita toka Urumi(Roma) Julius Caiser aliwavamia maadui zake na kuwapga kwa kusafil umbali mrefu,alipofika ktk himaya ya adui aliua na kuteketeza kila kilicho cha adui..kufikisha ujumbe kwa walio Rome na Senator J.Caiser alisema "Veni,Vidi,Vici" = "I came,I saw,I conquered"..
Hii ndo ikawa alama ya ushindi,na J.Caiser alipopita mbele za watu alikunja vidole kwa alama ya V kama tafsiri ya ushindi,na askari wote waliopgana ktk vita hvyo waliwekewa alama ya "V" tatu ktk mabega yao kama alama ya ushujaa,na t oka hapo V ikawa alama ya cheo ktk jeshi...kumbe alama ya V kwa Chadema si ushetani,haina mahusiano na mashetani...ni alama ya "Victory"...mashabiki wa mpira hutmia,wachezaji na hata makocha wao(japo wengine hufikili kuwa wanamanisha watashnda goli mbili).,si Chadema peke yao!
JAMBO LEO Lisigeuke kuwa udaku,lisidhalilishe dini na viongozi wa watu,wajiheshimu!Wasitumike..k una mbinu nyingi za kuibana Chadema lakn si kwa mtindo huo!kweli Chadema imewabana na bado kidogo mtaachia...NAWASILISHA.
Fredrick Katulanda.
CHANZO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni