Alhamisi, 19 Aprili 2012
Wajasiriamali Wasaidiwa Iringa
TAASISI ya Sekta Binafsi ya Tanzania (TPSF) kupitia mradi wake wa Business Development Gateway (BDG) imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 2,413,6000 kwa wajasiria mali 1,576 katika mikoa ya 26 ya Tanzania Bara na visiwani.
Akizungumza leo kwa niaba ya mkurugenzi wa TPSF ,Bw Godfrey Macha wakati sherehe ya kuwakabidhi hundi yenye tahamani ya shilingi milioni 67.4 wajasiriamali washindi wa Programu ya fanikiwa kibiashara (BDG ) mkoani Iringa ,alisema kuwa fedha hizo ni sehemu ya fedha zote kiasi cha zaidi ya bilioni 2 ambazo zimetolewa hadi sasa na BDG hapa nchini.
Alisema kuwa fedha hizo zimetolewa wajasiriamali waliopata alama za juu katika mafunzo na majaribio ya ujasiriamali yanayoendeshwa nchi nzima kupitia mradi wake wa Business Development Gateway Programme (TPSF-BDG) Macha alisema kuwa kati yao wajasiriamali 1,576 waliopata mbegu mtaji wa asilimia 56 ni wanawake na asilimia 43 ni vijana chini ya miaka 35. Hata hivyo alisema kuwa washindi wamepata mbegu mtaji za kati ya shilingi milioni 1.1 hadi milioni 2.8 kila mmoja.
Alisema kuwa katika kipindi cha miezi mitano kuanzia Januari mwaka huu wajasiriamali 2,100 waliokidhi vigezo wamefundishwa na kushindanishwa kwa vitendo vya kujenga UJASIRIAMALI. Wengi wamerasimisha biashara na kulipa kodi zao katika kipindi hicho.
“TPSF inashirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID) ambalo limetoa takribani shilingi bilioni 17 kwa ajili ya kutoa mafunzo, kusimamia mradi na kuwapa washindi mbegu mtaji.
Zoezi la utoaji zawadi linafanywa kila mkoa katika mwezi Juni na Julai. TPSF inashirikiana na Serikali na DFID katika zoezi la kutoa zawadi”alisema Macha
Kuwa washindi 1,576 wamejishindia shilingi bilioni 2.4136 mpaka sasa na bado mafunzo na majaribio yanaendelea na watakaofanya vizuri zaidi, watapata mbegu mtaji zaidi ambapo washindi wa juu kabisa wataweza kujishindia hadi mbegu mtaji za shilingi milioni 30.
Aidha alisema kuwa Agosti mwaka huu TPSF itakuwa imegawa mbegu mtaji za shilingi bilioni 5.62 na washindi hao wa juu kabisa watepewa mbegu mtaji zao katika maonyesho na sherehe maalum zitakazofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam hapo mwezi Agosti mwaka huu kwa kukabidhiwa fedha hizo na waziri mkuu Mizengo Pinda ambaye ndie anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Alisema kuwa katika kufanikisha programu hiiyo TPSF-BDG inashirikiana na SIDO, ZNCCIA, TCCIA, NMB, PBZ, COSTECH and ZIFA.
Kwa upande wake Mwakilishi wa benki ya NMB Boniface Munyi
akizungumza kwa niaba ya meneja wa Benki hiyo tawi la Mkwawa Iringa alisema kuwa benki hiyo itaendelea kuwa pega kwa bega ya wajasiriamali hao na kuwataka kutotumia vibaya fedha hizo za mitaji na badala yake kuafungua akaunti ambayo ni maalum kwa ajili ya shughuli zao hizo .
Kaimu Meneja wa SIDO mkoa wa Iringa Niko Mahinya alisema kuwa SIDO mkoa wa Iringa imeendelea kuwawezesha wajasiriamali kwa kupata mafunzo maalum ya ujasiriamali na kuwa idadi kubwa ya wajasiriamali ambao wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali wameendelea kufanya vema katika uzalishaji wa bidhaa zao.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo afisa biashara wa Manispaa ya Iringa Ipyana Kabuje aliwataka wajasiriamali hao ambao wamepatiwa fedha hizo kuendelea kujituma zaidi na kujiunga na BDG kama njia ya kujikwamua zaidi kiuchumi huku akiwataka kuzalisha bidhaa zenye ubora badala ya kuendelea kuzalisha bidhaa zisizo na ubora.
kwa upande wao Wajasiriamali mkoani Iringa wamesema kuwa jitihada zinazofanywa na taasisi binafsi ya PTSF- DBG hapa nchini zimeendelea kuwakomboa kiuchumi kwa wao kuongeza kasi ya uzalishaji zaidi .
Wakizungumza mara baada ya sherehe fupi ya kukabidhiwa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 67.4 mjasiriamali Michael Mlole alisema kuwa pamoja na awali kuanza katika hali ya kusuasua kazi hiyo ya ujasiriamali ila baada ya kupatiwa mafunzo ya DBG na kuwezesha wameendelea kukua zaidi kibiashara na hivyo kupongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya hapa nchini.
Kwani alisema kuwa hivi sasa wajasiriamali hao ambao awali walikuwa wakiitwa ni wajasirimali wadogo kwa sasa wao wanajiona kuwa ni wafanyabiashara wakubwa kutokana na uwezeshaji unaofanyika chini ya DBG .
Chanzo:Francis Godwin
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni