.........BLOG HII BADO IPO KWENYE MATENGENEZO......

Jumatano, 1 Juni 2011

USALITI WA NDOA KATIKA MAISHA

Ni wazi kabisa kwa asilimia kubwa baadhi ya wanaume huwasaliti wenza wao pindi wanapopata ujauzito, leo nilikuwa nazungumza na mama mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe amenisimulia namna ambavyo mume wake aliweza kumsaliti kipindi akiwa mjamzito tena huku akimuonyesha wazi amesema "kiukweli wanawake tunakutana na matatizo mengi sana katika ndoa mimi mume wangu kipindi nikiwa mjamzito alianza kunifanyia vituko vya kila aina mwanzoni mimba ikiwa na miezi mitatu hadi mitano kidogo ilikuwa afadhali anarudi nyumbani mapema tunalala pamoja.

lakini ilipofika miezi sita na kuendelea mambo yalibadilika akawa analala nje akirudi amelewa nikimuuliza kwa nini ananifanyia hivyo ananijibu kuwa ni muda wake wa kufurahi kwani mimi siwezi kumridhisha kwa lolote kutokana na hali niliyonayo, nilitamani kuondoka lakini ndugu zangu walinishauri nivumilie,nilipata mateso kwa muda mrefu hadi nilipojifungua ndipo tabia yake ilianza kubadilika alianza kuwahi kurudi nyumbani huku akiniomba msamaha kwa yaliyotokea, nimemsamehe lakini wakati mwingine huwa najiuliza je nikibeba tena ujauzito atarudia tabia yake ya zamani?? "Nawashauri akina baba wawe na roho ya huruma kipindi mama akiwa mjamzito ndiyo anahitaji msaada wako zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni