Jumanne, 24 Aprili 2012
AJALI AJALI AJALI
Abiria zaidi ya 40 wamenusurika kifo baada ya basi waliokuwa wakisafiri aina ya Coaster, lenye nambari za usajili T 374 AVR, kupinduka lilipogongwa kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa basi la El Saedy likiwa katika hali ya mwendokasi liliharibika mfumo wa breki kutoka eneo la Mlima Nyoka na kuligonga basi hilo dogo kwa nyuma katika mteremko wa Shule ya Sekondari Imezu, hali iliyopelekea basi hilo dogo kupinduka.
Baada ya Coaster kupinduka basi la El Saedy likiwa bado katika mwendokasi liliendelea na safari, kabla ya dereva kufanikiwa kulichepusha kabla halijavuka reli ya TAZARA katika Kijiji cha Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Aidha baadhi ya abiria katika basi hilo dogo walikuwemo wanafunzi 28, wa kike na kiume wakielekea shuleni majira ya saa moja asubuhi, Aprili 23 mwaka huu katika Shule ya Sekondari Imezu.
Mara baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya abiria walikuwemo katika basi hilo dogo walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya, ambapo kati yao wamelazwa ili kufanyiwa uchunguzi na wengine wakiruhusiwa kurudi nyumbani.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mbeya Barakiel Masaki,hakupatikana kuelezea ajali hiyo ingawa dereva wa basi la El Saedy anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.
Wakati huo huo watroto watano waliokuwa wakioga katika mfereji wa Mwanjejele, uliopo Igurusi Wilaya ya Mbarali, Aprili 22 mwaka huu majira ya saa tisa alasiriwaliokota begi lililokuwa linaelea katika maji ya mfereji huo na kukuta maiti ya mtoto mchanga.
Maiti hiyo ikiwa imeharibika vibaya kutokana na kuoza ndipo walipolichukua begi hilo na kulikabidhi katika Kituo cha Polisi cha Igurusi.
Hata hivyo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo, licha ya wimbi la kuuawa kwa watoto wachanga Mkoani Mbeya limekuwa tatizo hali inayosababisha vifo kwa watoto wasio na hatia.
P
Jumapili, 22 Aprili 2012
LOWASSA ACHANGIA MIL. 10 KWA UJENZI WA KANISA - MBEYA
WAZIRI mkuu aliyejiuzulu,Edward Lowassa ametoa Shilingi Milioni 10 taslimu kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la EAGT lililopo mjini Tunduma wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Fedha hizo amezitoa wakati wa harambee ya kuchagia ujenzi wa kanisa hilo ililofanyika katika viwanja vya Hoteli ya High Class mjini hapa.
Lowassa ambaye alitumia takribani dakika 28 pekee kuwepo katika viwanja hivyo, alisema kuwa watanzania ni vema wakawa na wito wa kujenga nyumba za kuabudia kuliko kujenga nyumba za starehe zikiwemo Bar.
‘’Nafurahi kualikwa katika tafrija hii na niwaombe kwa pamoja tuwe na tabia za kujenga nyumba za Mungu ambazo zitakusanya waumini kuabudia na kuomba kwa pamoja kuliko hivi ilivyo wengi wanajenga Bar’’ alisema Lowassa.
Aliongeza kuwa kwa sasa nchi ipo katika kipindi kigumu cha uchumi na masuala ya katiba mpya hivyo aliwaomba wakristo kupanga ratiba ya kuiombea nchi ili iendelee kuwa na amani na watanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na umoja uliopo.
Alisema kuwa jambo hilo ni muhimu kwa kila mtanzania ambapo kila mmoja aliombee taifa,ili lisikumbwe naghasia na mambo kama yale yanayotokea katika nchi zingine ikiwemo Nigeria ambako kikundi cha Boko Haramu hakiwataki Wakristo.
‘’Mimi ,familia yangu na marafiki zangu tumeguswa na ujenzi wa nyumba ya Mungu na tunatoa Shilingi Milioni 10 na huu ni mwanzo tu’’ alisema Lowassa.
Sanjari na kutoa fedha hizo, pia alimuomba askofu wa kanisa hilo aandae tamasha la kuchagia ujenzi huo kwa kwaya zote ambazo zilihudhuria harambee hiyo na kwamba kwaya tatu zitakazoshinda zitachagua mwakilishi mmoja ambao atawagharamia kwenda nchini Israel kuona historia ya kikristo.
Alisema amefanya hivyo kwasababu anapenda sana uimbaji na kwamba alibarikiwa zaidi alipoimba pamoja na wanakwaya hao wimbo usemao ‘’Bwana Mungu nashangaa kabisa nikitazama jinsi ulivyo.
Kwa upande wake Askofu mkuu wa Kanisa hilo,Keneth Kasunga alimshukuru Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli kuwa amejenga nyumba ya Mungu na wala si ya Mtu binafsi hivyo Mungu hawezi kumuacha katika mambo yake yote na mahitaji pia.
Kanisa hilo lilisema kuwa katika ujenzi wa kanisa hilo lenye waumini 750, walipungukiwa kiasi cha Shilingi Milioni 750, kanisa litakaloweza kuwaondolea adha waumini ambao wanasali wakiwa nje kutokana na kanisa lililopo kwa sasa kuwa dogo.
CHANZO

Jumamosi, 21 Aprili 2012
Wabunge wa CCM watishwa
Katika hatua nyingine, imedaiwa kuwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi, wameitwa na kutishwa kuchukuliwa hatua ikiwa watasaini azimio hilo.
Mmoja wa wabunge wa CCM aliyekiri kuitwa ni Deo Filikunjombe (Ludewa) ambaye alisema alilazimika kusaini kabla ya kuitikia wito huo.
Filikunjombe, alikiri kuitwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, na kumtaka kutosaini azimio hilo, lakini akamwambia alikwishasaini na alifanya hivyo kwa niaba ya wananchi wa Ludewa ambao wamechukizwa na ubadhirifu mkubwa uliofanywa na watendaji hao wa serikali.
Kuhusu wabunge wa CCM kutosaini azimo hilo, Filikunjombe alisema kanuni haikusema wabunge wote, kwani inafahamika wengine wanarudi nyuma alisema.
Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde alisema suala la hoja ya kikanuni ina lengo la kuchelewesha mchakato wa kuwaondoa wanaolalamikiwa na kuahidi kuwaondoa hata kama Bunge litawakingia kifua.
Alisema kama mawaziri wanaolalamikiwa wataendelea kubakia katika nafasi zao ni bora wabunge wa CCM wakaondoka na kuwaachia wao majukumu yote.
Alipoulizwa kama msimamo wake hauwezi kuwakera viongozi wake na kuamua kumchukulia hatua ikiwa ni pamoja na kumuondoa katika chama, Lusinde alisema kuwa hilo halihofii kwa kuwa hana hati miliki ya ubunge wa Mtera na zaidi ataendelea kubakia Mtanzania anayepigania maslahi ya nchi yake.
Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM), alisema katika mapendekezo yaliyoafikiwa juzi hakuna azimio katika kamati yoyote lililotaka waziri aondolewe na kusema kuwa alichokuwa akikifanya Zitto ni usanii.
“Katika taarifa yake ile alipaswa aseme Bunge limependekeza mtu fulani awajibishwe, hivyo alitakiwa kuleta nyongeza katika taarifa yake. Hakuna aliyeleta. Ile ni burudani tu,” alisema na kuongeza kuwa hoja hiyo haina mashiko.
Alihoji kuwa iwapo Pinda alishindwa kumuondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, atawezaje kumuondoa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo.
Alisema kuwa ili hoja hiyo ifanikiwe ni lazima Spika aridhike kwamba ilifuata taratibu na ina sifa hata ikisainiwa na wabunge 200 kama haina sifa haiwezi kupita.
CHANZO
Ijumaa, 20 Aprili 2012
ALICHOKUTANA NACHO AY KWENYE SHOW SUDAN KUSINI.
Baada ya kurudi Bongo akitokea Sudan Kusini alikokwenda kupiga show kwa mara ya kwanza japo wamekua wakimwalika toka zamani, AY amesema kwamba hakua na hofu yoyote kwenda kwenye hiyo nchi ambayo iko vitani.
Amesema “ulinzi ulikua mzuri kwangu nilikua nalindwa karibu na askari nane ambao wote wana AK 47 poamoja na convoy, nilikua nalindwa mimi pamoja na watu wangu wanne nilioenda nao, tulikua tunalindwa mpaka usiku tunapokwenda kulala”
Baada ya kufanya show ya kwanza Ay amesema jamaa waliikubali sana ikabidi wamwalike kwenye show nyingine ya pili ambayo ingefanyika kesho yake lakini ikashindikana baada ya kupokea simu kutoka jeshini kwamba vita imeanza hivyo kila kitu kikasimama, simu zikakatwa network, umeme hakuna, ndege za kivita zikasikika huku wanajeshi wakipita kwenda vitani.
Ay alipiga show alhamisi iliyopita huko Juba Sudan Kusini ambapo baada ya show ya pili kufutwa, jamaa wakamkabidhi mkwanja wake na kesho yake asubuhi wakamsindikiza mpaka Airport lakini wamemualika tena kwenye show nyingine mbili ikiwemo moja miezi minne ijayo katika sherehe za Uhuru ambazo zimeandaliwa na serikali.
Kwa furaha AY amesema “moja kati ya vitu nilivyokutana navyo vikamshangaza ni pale ambapo nilikua nakula usiku likapita kundi la wanajeshi alafu wakasema wewe ni AY wewe tunakujua wewe, hata alienipeleka Sudan alishangaa… wale wanajeshi wakaniuluza tena wapi mwanaFaa wakimaanisha Mwana FA, nikasema ahhh kumbe hata mgosi nae wanamtambua………. kingine ambacho kimenishangaza zaidi ni kwamba hela yao ni kubwa kuliko ya nchi yeyote Afrika Mashariki”
Alhamisi, 19 Aprili 2012
Jinamizi La Millya: Diwani Wa CCM Mwanza Ajiunga CHADEMA
UPEPO mbaya unaonekana kukikumba Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa viongozi wake kukihama chama hicho, umeingia katika Mkoa wa Mwanza, ambapo Diwani wa Kata ya Nyampulukano Wilayani Sengerema mkoani hapa, Hamis Mwangao Tabasamu ametangaza kuihama CCM na kujiunga na Chadema.
Diwani huyo ambaye amejipambanua kwa kupiga vita ufisadi ndani ya wilaya hiyo, ametangaza azma yake hiyo katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika Ryan's hoteli, na kupokelewa na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema).
Diwani Tabasamu ambaye jumamosi amepanga kuhudhuria na kuhutubia mkutano mkubwa utakaoongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa kata ya Nyampulukano, amekuwa ni miongoni mwa viongozi wengine wa CCM kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema ndani ya muda wa wiki moja.
Hivi karibuni, aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mkoa wa Arusha, James Milya alitangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote kisha kujiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Mbali na Milya, viongozi wengine kadhaa akiwemo diwani wa Kata ya Sombetini mkoani Arusha, Alphonce Mawazo (CCM), juzi alikihama chama chake hicho kisha kujiunga na Chadema, chama ambacho kinaonekana kuiweka pabaya CCM na Serikali yake kwa ujumla.
Akizungumza mchana huu wa leo, katika kikao chake na waandishi mbele ya Lema ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa, diwani Tabasamu ambaye aliwahi kuibua tuhuma za ufisadi katika halmashauri ya Wilaya ya Sengerema alisema: "Kuanzia leo (jana), natangaza rasmi kukuhama CCM na kujiunga na Chadema".
Alisema, lengo lake la kuhama kutoka ndani ya CCM si la kushawishiwa na mtu ama kiongozi yeyote, bali ni dhamira yake ya kweli kama Mtanzania halisi mwenye uhuru wa mawazo, na kwamba amechoshwa na siasa za 'majitaka' ndani ya CCM.
Kwa mujibu wa diwani huyo wa Nyampulukano wilayani Sengerema, kuondoka kwake CCM inatokana na kushindwa kuafikiana katika maslahi ya wananchi, ambapo alidai wapo baadhi ya viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo wanakumbatia vitendo vya kifisadi.
"Uamuzi wangu huu wa kuhamia Chadema kutoka CCM unatokana na kushindwa
kuafikiana katika mambo yanayogusa maslahi ya wananchi katika
halmashauri ya wilaya ya Sengerema.
"Mafisadi wameliteka baraza la Madiwani la Sengerema!. Kwa maana hiyo natangaza rasmi leo, najiuzulu nafasi zangu zote ndani ya CCM, na nahamia Chadema", alisema Tabasamu ambaye amewahi kuingia mgogoro na mkuu wa wilaya hiyo, Elinas Palagyo kwa kile kinachodaiwa msimamo wake wa kupiga vita ufisadi.
Alizitaja sababu nne za kuhama ndani ya chama hicho tawala kuwa ni pamoja na kuwepo kwa madiwani wengi wa CCM wasio wazalendo kwa kuruhusu kuhamishwa mnada wa ng'ombe kutoka Kijiji cha Ibondo Nyampulukano kisha kuhamishiwa Kata ya Sima.
Sababu nyingine ni ucheleweshaji wa makusudi kuunda halmashauri ya mji
wa Sengerema kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka huu, kupunguzwa kwa mipaka ya mji mdogo bila kufuata vikao halali vya kisheria.
Nyingine ni halmashauri ya wilaya hiyo ya Sengerema, iliyopo chini ya uenyekiti wake, Mathew Lubongeja (CCM), kushindwa kuwachukulia hatua watu aliowaita wezi waliotajwa na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), PPRA, ambapo alidai maelekezo ya CAG kuhusu kuchukuliwa hatua watuhumiwa wa ufisadi kutotekelezwa hadi leo.
Awali, akizungumza katika kikao hicho na waandishi wa habari, Lema alimpongeza diwani huyo wa Nyampulukano kwa kuondoka ndani ya CCM na kujiunga na Chadema, na alisema huo ni uamuzi sahihi na wa kijasiri unaolenga kuikomboa nchi hii kutoka CCM.
"Nakupongeza sana mheshimiwa Tabasamu kwa kuondoka CCM na kuja Chadema chama makini. Nawaomba sana na madiwani, wabunge na viongozi wengine wa CCM wawahi kujiunga na Chadema kabla safina haijafungwa", alisema Lema.

Airtel yatoa compyuta na vitabu vya milioni 25/- TZS chuo kikuu cha Dodoma

Mkuu wa wilaya ya Bahi Bi Betty Mkwasa, akiwa na Makamu Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM) jana pamoja na wafanyakazi wa Airtel na baadhi ya wanafunzi wa IT chuoni hapo wakiwa wameshikilia vitabu vilivyotolewa msaada na Airtel kwa chuo hicho wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye thamani ya milioni 25/- TZS toka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini.
IDARA YA UHAMIAJI MKOANI IRINGA YAWAKAMATA RAIA WAEPHIOPIA 38
Idara ya uhamiaji mkoa wa Iringa imefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wahamiaji haramu 38 ambao walikuwa wakitoa nchini Ephiopia kuelekea Afrika ya kusini.
Watuhumiwa hao wamekamatwa leo katika Msitu wa Sao Hill wilaya ya Mufindi baada ya mwenyeji wao kuwatelekeza katika msitu huo kwa madai ya kushindwa kuongeza malipo ya kuwavusha kwenda Afrika ya kusini .
CHANZO
MAGONJWA MENGI HUSABABISHWA NA UHARIBIFU WA TABAKA LA OZONE
Kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya ngozi,uharibifu wa macho maarufu kwa jina la mtoto wa jicho, na upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi, kumeelezwa kuwa husababishwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa tabaka la ozone ambapo kunatokana na shughuli za kibinadamu kama vile matumizi ya kemikali haribifu na zisizo rafiki kwa mazingira.
Hayo yameelezwa leo Mjini Arusha katika hotuba ya ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya mafundi mchundo wa majokofu na viyoyozi kuhusu teknolojia mbadala ya majokofu na viyoyozi, iliyosomwa na Afisa Mazingira wa Mkoa bw.Julius Achiula kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa.
Akisoma hotuba hiyo,Bw. Achiula ameainisha baadhi ya chemikali hizo kuwa ni methyl bromide, halons na chloroflorocarborns ambazo hutumika kama vipozi katika mafriji, viyoyozi, vifaa vya kuzima moto, usafishaaji chuma, ufikizaji wa mazao katika maghala na utengenezaji wa magodoro ambazo huleta madhara kwa tabaka la ozone na adhari zake hotokea kwa binadamu, mimea na viumbe hai.
Uhifadhi wa tabaka la ozone umetokana na utekelezaji wa Mkataba wa Montreal na Vienna ambayo Tanzania ni mwanachama.
Warsha hiyo inayoratibiwa na Ofisi ya makamu wa rais imehusisha washiriki kutoka, baraza la taifa la Hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC, chuo cha ufundi VETA Moshi, wanahabari, maafisa mazingira wa mkoa wa arusha na mafundi mchundo.
CHANZO
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)